Menu ›
Biashara
Tue, 7 Mar 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Ubalozi wa Tanzania Nchini China umesema mkataba wa kuruhusu asali kutoka Tanzania kuingia katika soko la China utasainiwa hivi karibuni.
Taarifa ya Ubalozi huo leo imesema hili ni utekelezaji wa makubaliano ya kukuza biashara kati ya Tanzania na China yaliyofikiwa wakati wa ziara ya Rais Samia nchini China.
Mkataba huu utafungua fursa kwa Wafanyabiashara wa asali Nchini Tanzania ambao wamekuwa na kiu hiyo kwa muda mrefu.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live