Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ardhi mikoa minne yakosa virutubisho vya kilimo

Kilimo Kilimanjaro Ardhi mikoa minne yakosa virutubisho vya kilimo

Sun, 20 Feb 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Utafiti wa ardhi kwa ajili ya kilimo uliofanywa na jopo la watafiti katika mikoa minne umebainisha kuwa asilimia 60 hadi 70 ya udongo katika mikoa hiyo umepoteza virutubisho vingi hali inayopelekea wakulima kushindwa kupata mavuno mengi.

Mikoa iliyofaanyiwa utafiti ni pamoja na Mbeya, Morogoro, Iringa na Rukwa kwa mazao ya mahindi, alizeti, viazi na mpunga hali inayosababisha wakulima kutumia nguvu nyingi kwa kuambulia mavuno kidogo.

Akizungumza wakati wa kuwasirisha ripoti ya utafiti huo kwa mkoa wa Morogoro, Mtafiti wa Udongo Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (Tari) Uyole, Fredrick Mlowe amesema utafiti huo umefanyika katika vijiji 400 katika mikoa minne na kubaini kuwa virutubisho vya msingi katika udongo vimepotea kutokana na matumizi mabaya ya aridhi.

“Ukosefu wa kirutubisho cha zinki katika udongo kwa kilimo cha mpunga inapelekea mkulima kukosa mavuno kwa asilimia 30 mpaka 35 na kirutubisho cha Sulpha katika udongo mkulima pia anaweza kukosa mavuno kati ya 70% kutokana na ardhi hii minne imechoka sana.”amesema Mlawe.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Kilimo (Tari) Uyole mkoani Mbeya, Dk Tulole Lugendo amesema licha ya udongo kutokuwa na virutubisho vya kutosha bado mazao mengine yanaweza kulimwa katika mikoa hiyo na mkulima kuinuka kiuchumi.

Dk Lugendo amesema katika utafiti huo wamegundua upo uwezekano wa kuanzisha mazao mapya yasiyozoeleka ya michikichi, kokoa na makadamia na wakulima wakapata faida katika kilimo.

Advertisement Akipokea taarifa ya ripoti ya utafiti huo kwa mkoa wa Morogoro, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mipango na Matumizi Bora ya Ardhi, Wizara ya Kilimo, Mhandisi Juma Mdeke amesema wizara hiyo itaendelea kushirikiana na wadau wa kilimo nchini ili kukifanya kilimo kiweze kuwanufaisha wakulima na taifa kwa ujumla.

“Utafiti huu uliopatikana utumike kwa wakulima kuujua kwani dhamira ya wizara ni kukakikisha ifikapo mwaka 2030 kuwepo na chakula cha kutosha na hatuwezi kuwa na chakula cha kutosha kuwepo kwa wakulima wanaoendelea kulima kizamani.”amesema Mhandisi Mdeke.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz