Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ansaf yataja suluhisho la changamoto tano za Kilimo

59355 Teknolojiapic

Fri, 24 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa huru la Kilimo (Ansaf), Audax Rukonge amesema licha ya Tanzania kuwa na fursa ya idadi ya watu na masoko ya kilimo, bado inakabiliwa na sera zisizotabirika kwa wawekezaji.

Akizungumza katika jukwaa la Fikra la MCL leo Alhamisi Mei 23, 2019 Jijini Dar es Salaam, Rukonge amesema

 mazingira pia utozwaji wa kodi si rafiki.

“Kwa sasa tuna taasisi, kama unataka kuwekeza kwenye maziwa unahitaji kujisajili kwa taasisi hadi 26. Tutumie teknolojia ili ikiwezekana wajisajili mitandaoni.

“Kutotabirika kwa Sera pia kuna athiri uwekezaji. Kwa mfano kuna miradi ya umwagiliaji, kama umeshawekeza halafu Sera zinabadilishwa inakuwa hasara," amesema.

Hivyo, amesema kuna haja ya kuwasaidia  wawekezaji wa ndani kwa sababu mcheza kwao hutunzwa.

Pia Soma

“Tuwasaidie katika eneo la kodi, hao ndiyo hutoa ajira kwa wananchi."

Amesema kuna vijana kati ya 800,000 hadi milioni moja wanaomaliza vyuo kila mwaka wakitafuta ajira, hivyo ni lazima kuwe na Sera wezeshi.

Kuhusu huduma za ugani, amesema pamoja na uwiano wa kijiji kimoja mgani mmoja, wagani hao hawatoshi hivyo amesema kuna haja ya kuwekeze zaidi kwenye teknolojia.

“Kuwe pia na kozi kwa maofisa ugani, wengine hawajapata mafunzo tangu wamalize shule,” amesema Rukonge.

Kuhusu utunzaji wa mazao yanayovunwa, Rukonge amesema kati ya asilimia 35-40 ya mazao ya nafaka hupotea baada ya kuvunwa, huku asilimia 60 ya matunda na mboga yanaharibika, hivyo akashauri kuimarishwa kwa teknolojia ili kuepusha hasara.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz