Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Almasi ya Ajabu Kutoka Angani Yapigwa Mnada

QALMASI ANGANI Almasi ya Ajabu Kutoka Angani Yapigwa Mnada

Thu, 3 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Almasi nyeusi yenye umri wa mabilioni ya miaka inayodhaniwa kuwa imetoka anga ya juu inapigwa mnada.

Almasi hiyo iliyoitwa The Enigma, inaaminika kuwa almasi kubwa zaidi iliyokatwa duniani na huenda ilitokana na athari ya kimondo.

Katika karati 555.55 jiwe hilo linachukuliwa kuwa nzito sana kuwa almasi, yenye uzani sawa na ndizi.

Jiwe hilo linatarajiwa kuchuma zaidi ya pauni milioni 4.4 katika mnada wa Sotheby mjini London wakati zabuni ya mtandaoni itafungwa wiki ijayo.

Jiwe hilo i ni carbonado, mojawapo ya aina ngumu zaidi za almasi ya asili.

Almasi nyeusi kawaida huwa na umri wa miaka bilioni 2.6 hadi 3.2 - wakati kabla ya dinosaria kuwepo.

Dunia yenyewe ina umri wa miaka bilioni 4.65, kwa hivyo si kubwa zaidi kiumri kuliko almasi nyeusi.

Carbonados ni nadra sana na zimewahi kugunduliwa tu nchini Brazil na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Kwa sababu zina osbornite, madini yanayopatikana tu kwenye vimondo, vinaaminika kuwa vinatoka angani. Lakini asili yake haswa haijulikani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live