Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyesifiwa bungeni apandishwa cheo CRDB

Mon, 20 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Huwa ni furaha kwa kila mgeni anayealikwa kuhudhuria vikao vya Bunge jijini Dodoma lakini imekuwa maradufu baada ya Grace Adam ambaye kutokana na pongezi alizopewa na wabunge, mwajiri wake amempandisha cheo leo Jumamosi Mei 18, 2019.

Grace, ofisa wa Benki ya CRDB akiwa na wenzake watatu walialikwa bungeni wiki mbili zilizopita na Spika Job Ndugai alipowatambulisha, Bunge lililipuka kwa shangwe.

Wakati anawatambulisha, Ndugai alisema wageni hao wanne ni maofisa uhusiano kwa wateja maalumu na waliongozwa na Agusta Mfuru.

Baada ya utambulisho huo, wabunge walipiga makofi mengi na spika akasema ni kwa ajili ya Grace. “Tunaomba timu inayotoka makao makuu mpeleke salamu za Bunge kwa uongozi wa CRDB kwa kazi nzuri anayofanya Grace. Anastahili kupandishwa cheo, ni mfanyakazi bora kwa makofi haya.”

Huenda spika alikuwa anatania lakini ujumbe umefika mahali husika na leo Mei 18, 2019 kwenye mkutano mkuu wa 24 wa benki hiyo, mkurugenzi mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela ametangaza kumpandisha cheo ofisa huyo.

“Tunapoona mtu au taasisi anapongeza huduma zetu, nasi huwa tunachukua hatua. Hivi karibuni wabunge na spika walipongeza huduma wanazopata kupitia tawi letu lililopo kwenye viunga vya Bunge na wakamtaja Grace kutokana na kazi nzuri anayoifanya. Nasi tumeliona hilo na tumempandisha cheo,” amesema Nsekela.

Pia Soma

Licha ya kumpandisha cheo bila kutaja atakuwa meneja wa tawi gani kati ya 266 yaliyopo nchini Tanzania, alimkabidhi bahasha yenye bakshishi yake pamoja na barua ya kupandishwa wadhifa.

“Ndani ya bahasha hii kuna barua yake ya kupandishwa cheo na zawadi ya menejimenti kwake,” amesema Nsekela.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz