Staa wa Bongo Fleva, King Alikiba, kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema Kilimo ni eneo jingine ambalo amewekeza ukiacha muziki.
Amesisitiza kuwa kama unataka kupiga mkwanja, basi unapatikana kwenye kilimo. Alikiba amekiri kuwa kwenye kilimo kuna uhakika na kinaweza kubadili maisha ya vijana wengi. Ame-share kuunga jitihada za Bi-Mkubwa kwa vijana.
Siku za karibuni watu wengi wameanza kujiingiza katika kilimo kutokana na juhudi ambazo serikali kupitia Wizara ya Kilimo imekua ikizifanya kuboresha sekta hii ambayo kipindi cha nyuma ilionekana ni ya watu wa mikoani au vijijini.
Kwa sasa, wafanyabiashara, wasanii na vijana wameingia kwa wingi kwenye kilimo. Mwezi uliopita wizara ya Kilimo chini ya Waziri wake @bashehussein alichagua vijana 812 kuingia kwenye program ya Buiding Better Tomorrow (BBT) ambapo watapatiwa mafunzo, mikopo na misaada kwa vijana waliojitosa kwenye sekta ya kilimo.