Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Algeria, Nigeria na Niger zakubaliana kuuza gesi Ulaya

Gas Pipeline Algeria, Nigeria na Niger zakubaliana kuuza gesi Ulaya

Sat, 30 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wqziri wa nishati wa Algeria, Niger na Nigeria wametia saini makubaliano juu ya ujenzi wa bomba la gesi kupitia kwenye jangwa la Sahara ili kupeleka gesi barani Ulaya.

Baada ya ujenzi kukamilika bomba hilo la kilometa 4000 litakuwa na uwezo wa kupeleka mita bilioni 30 barani Ulaya kwa mwaka.

Bomba hilo litajengwa kwa gharama za dola bilioni 13 litaanzia Nigeria na kupitia Niger hadi Algeria. Na kutokea hapo gesi itapitishwa kwenye bomba la chini ya bahari ya Mediterrania hadi Ulaya au itapakiwa kwenye matanki ya gesi ya kioevu na kusafirishwa hadi barani Ulaya.

Nchi za Umoja wa Ulaya zinakusudia kuondokana na kuitegemea Urusi kwa ajili ya mahitaji ya nishati. Rais wa halmashauri ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amesema lengo la mradi huo ni kuepuka nchi za jumuiya hiyo kushinikizwa na Urusi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: