Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Akaunti za Twitter zapoteza wafuasi

Twitter Wafuasi Akaunti za Twitter zapoteza wafuasi

Wed, 27 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu muhimu wa mrengo wa kushoto, akiwemo Barack Obama, wamepoteza maelfu ya wafuasi tangu bilionea Elon Musk aanze mpango wa kuununua mtandao wa kijamii wa Twitter, wakati idadi kubwa imefurika kwa wanasiasa wa mrengo wa kulia.

Musk, mtu tajiri kuliko wote duniani, alikamilisha mpango wa kujununua mtandao huo wa kijamii Jumatatu kwa dola 44 bilioni za Kimarekani (sawa na Sh102.3 trilioni za Kitanzania).

Habari hizo zilipokelewa kwa shangwe na mashabiki wa Musk, ambaye anajiita mtu anayependa uhuru usio na mipaka wa kuongea, huku ukiudhi watu wanaopigania uwepo wa udhibiti katika upotoshaji habari na maneno ya chuki.

Ahadi za kuhama mtandao huo zilizagaa zikiwa na kaulimbiu ya #LeaveTwitter (ondoka Twitter). Ndani ya saa chache, wengi walionekana kufuata kampeni hiyo.

Rais wa zamani wa Marekani, Obama, ambaye ndiye maarufu kuliko wote Twitter akiwa na wafuasi milioni 131, alipoteza watu 300,000 kati yao kwa usiku mmoja, kwa mujibu wa televisheni ya NBC.

Mbunge mtata wa chama cha Republican, Marjorie Taylor Greene, kw akulinganisha na Obama, alipata wafuasi 100,000 kwenye akaunti yake ya kibunge ya Twitter ndani ya saa 24.

Advertisement Greene, mshirika wa Donald Trump asiye na woga wa kuzungumza na ambaye alizuiwa katika mtandao huo, alisifu mpango huo wa kuinunua Twitter.

Alisema uamuzi huo unampa matumaini ya kurejeshewa akaunti yake ya Twitter, akirejea mfumo wa uhakiki wa mtandao huo.

Twitter ilisema jana Jumanne ilipoongea na AFP kuwa wakati wanafuatilia mienendo hiyo, kupata au kupoteza wafuasi kunaonekana kuwa kwa kawaida na hasa kunatokana na akaunti mpya kufunguliwa na zilizokuwepo kufungwa.

Kuondoka kwa wafuasi kulikwenda mbali zaidi ya akaunti za kisiasa.

"Ni kitu cha kushangaza kupoteza wafuasi karibu 35,000 kwa usiku mmoja," akaunti ya Auschwitz ilisema jana. Akaunti hiyo ambayo ina wafuasi milioni 1.3 huchapisha picha na habari za waathirika wa kambini.

Musk amesema anataka kuongeza imanikwa Twitter, ambayo anaiona kama ni jukwaa la kidigitali la watu kutoa maoni yao kwa uhuru na kujadili.

Muasisi mwenza wa Twitter, Jack Dorsey alisema Jumatatu kuwa "mpango wa Elon wa kuanzisha jukwaa ambalo linaaminiwa kwa kiasi chote na shirikishi ni sahihi."

Alimsifu Musk na ofisa mtendaji mkuu wa Twitter, Parag Agrawal "kwa kuiondoa kampuni kutoka katika hali isiyowezekana.

"Hii ndio njia sahihi... Naiamini kwa moyo wangu wote."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live