Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Airtel yaahidi kutekeleza kanuni za vifurushi

2bc7d115007ff9da3b147285a2ce535b.png Airtel yaahidi kutekeleza kanuni za vifurushi

Fri, 5 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KAMPUNI ya simu ya Airtel Tanzania, imesema itatekeleza maagizo yaliyomo kwenye kanuni ndogo za mawasiliano kwa huduma za vifurishi zilizotangazwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

TCRA imetunga kanuni 13 zitakazoanza kutumika Aprili mwaka huu zikitaka kampuni za simu zinazotoa huduma huduma, kutoa taarifa kila wakati matumizi ya kifurushi yatakapofikia asilimia 75 na 100 kwa vifurushi vya muda wa maongezi, data na ujumbe wa maandishi (SMS).

Kanuni hizo pia zinamzuia mtoa huduma kupunguza kasi ya data kwenye kifurushi cha mteja ndani ya muda wa kifurushi husika wala hatatakiwa kufanya promosheni au kutoa ofa maalumu zaidi ya tatu kwa wakati mmoja kupitia huduma za sauti, data na SMS.

Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja Wakubwa wa Airtel, Boniface Mbwambo, aliliambia HabariLEO jana Dar es Salaam kuwa, kanuni hizo ni miongozo hivyo watazitekeleza.

“Mamlaka ya mawasiliano sisi tunafanya nao kazi na katika taarifa yao, wameelezea kwamba kanuni hizo zimetolewa kwa mujibu wa maoni pamoja na mapendekezo mbalimbali kutoka kwa wadau na watumiaji wa mawasiliano,” alisema Mbwambo.

Alisema TCRA imesikiliza maoni kutoka pande zote na kuleta kanuni hizo, hivyo watazizingatia katika utoaji wao wa huduma. Mbwambo alisema Airtel itaendelea kutoa huduma kwa uwazi na wameanza kutekeleza kanuni za mamlaka hiyo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz