Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania leo imezindua huduma inayojulikana kama ‘Tuma na ya Kutolea’.
Huduma hiyo itawawezesha wateja wa Airtel Money kutuma pesa kwa wapendwa wao, ndugu, marafiki pamoja na wanafamilia bila kukokotoa gharama ya hela ya Kutolea.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa kuzindua huduma hiyo, mkurugenzi wa Airtel Money Isaack Nchunda alisema uzinduzi wa huduma hiyo ni sehemu ya maadhimisho wiki ya huduma kwa wateja ilioanza Oktoba 7.
“Airtel imedhamiria kuendelea kuhakikisha ya kwamba inatoa huduma bora muda wote na hii ndio sababu tumekuwa tukiwaletea wateja wetu huduma na bidhaa ambazo ni za kiwango cha juu kabisa,’alisema Nchunda.
Aliongeza: Kwa muda mrefu, tumekuwa tukiona wateja wa Airtel Money wakituma pesa pamoja na ya ziada ambayo lengo lake ni kufidia gharama za Kutolea ambazo ni maarufu kama Tuma na ya Kutolea. Sisi nia yetu ni kuwapa wateja wetu kilicho bora, leo Airtel imekuja na huduma ambayo ni suluhishi wakati wa kutuma pesa kwani gharama za Kutolea zitakuwa zikikatwa wakati wa kutuma kwa kupitia menu ya Airtel Money.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano alisema, Airtel inatambua kuwa ni muhimu kuweka mahitaji ya wateja wetu mbele.
Pia Soma
- Simu za mkononi zinavyosaidia ukuaji wa biashara ndogo na za kati (SMEs) -nchini
- Mzumbe Dar es salaam yapewa cheti cha ubora mafunzo ya uhasibu wa juu
- Airtel yatangaza punguzo la simu katika wiki ya watoa huduma
Airtel kwa sasa inayo zaidi ya matawi 1,000 Airtel Money na mawakala wa Airtel Money zaidi ya 60,000 ambapo wateja wanaweza kupata huduma zote za Airtel kama vile kusajili kwa alama ya vidole, simu mpya za smartphone, vifaa vya simu pamoja huduma nyingine.
Caption: Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania Beatrice Singano akiongea na waandishi wa habari baada ya kuzindua huduma ya ambayo ni suluhisho kwa wateja wa Airtel Money.