Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Airport Arusha kuingizia Serikali mabilioni

Arusha City Airport Airport Arusha kuingizia Serikali mabilioni

Fri, 3 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Arusha, Eng. Elipid Tesha, amesema kukamilika kwa ujenzi wa jengo la abiria katika kiwanja hicho kutaongeza mapato ya kiwanja kutoka Tsh. Bilioni 2.8 hadi kufikia Tsh. Bilioni 6 kwa mwaka.

Akiongea mbele ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa ambaye alifika kukagua maendeleo ya ujenzi huo, Tesha amesema kukamilika kwa jengo hilo kutaruhusu kuhudumia abiria laki tano hadi sita kwa mwaka ambapo kwa sasa jengo lililopo linahudumia abiria laki mbili tu kwa mwaka.

Eng.Tesha amemuhakikishia Waziri Prof Mbarawa kuwa TAA itakamilisha jengo hilo kwa kuzingatia thamani ya fedha na ubora.

Jengo la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Arusha linagharimu kiasi cha Tsh. Bilioni 2.8 na limeshafikia asilimia 75 na linatarajiwa kukamilika mwezi Aprili mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live