Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Airbus mbioni kutua Dodoma

AIRTANZANIA Airbus mbioni kutua Dodoma

Mon, 22 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe, amesema kukamilika kwa upanuzi wa mita 250 katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma kutaruhusu ndege kubwa zenye uwezo wa kubeba abiria zaidi ya 200 aina ya Airbus kuruka na kutua kwenye kiwanja hicho.

Aidha, amesema zabuni kwa ajili ya kiwanja cha ndege cha Kimataifa cha Msalato imetangazwa na itafunguliwa mwezi Julai, mwaka huu ili kuendelea na utaratibu wa ujenzi.Waziri Kamwelwe alitoa kauli hiyo aliitoa juzi, jijini hapa mara baada ya kukagua maendeleo ya upanuzi huo unaotarajiwa kukamilika Agosti mwaka huu na ndege hizo kuanza safari zake Septemba mwaka huu.Alisema lengo la upanuzi huo ni kuruhusu ndege nyingi zaidi kutoa huduma kwa wakazi wa Mkoa wa Dodoma na mikoa ya jirani.

“Kiwanja hiki kiliongezwa urefu, lakini mahitaji yaliyopo sasa ni makubwa, tumelazimika kuongeza tena urefu ili kukidhi mahitaji kwani idadi ya watu inaongezeka kila siku kwa kuwa Dodoma ni Makao Makuu sasa ya Serikali," alisema.Waziri huyo alisema pamoja na upanuzi wa uwanja huo, Serikali imetangaza zabuni kwa ajili ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato."Pamoja na tatizo la ugonjwa wa corona (COVID-19) kuchangia ucheleweshaji wa ufunguaji na uchambuaji wa zabuni, Serikali inaendelea kuandaa mazingira ili mradi huo uanze," alisema.

Aidha, Waziri Kamwelwe alisema serikali ipo katika hatua za mwisho kukamilisha taratibu za ujenzi wa barabara za mzunguko jijini Dodoma (ringroad) zenye urefu wa kilometa 112 ambao utakuwa na makandarasi watatu.Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroads) Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Leonard Chimagu, alisema kulikuwa na tatizo la maji mengi, lakini wahandisi walipambana na kukabiliana na maji hayo kwa kuanza na uwekaji wa mawe makubwa kabla ya tabaka la kwanza ili kuimarisha barabara ya kuruka na kutua ndege."Mradi wa upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Dodoma, unafanywa na Kampuni ya CHICCO na unatarajiwa kukamilika Agosti mwaka huu na utagharimu kiasi cha Sh. bilioni 3.5," alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live