Kampuni ya Airbnb imewaambia wafanyakazi wake kuwa sasa wanaweza wakafanya kazi mbali na ofisini milele ikiwa watataka.
Wafanyakazi hao pia wanaruhusiwa kuhamia miji au maeneo yoyote wanayotaka ndani ya nchi wanazofanyia kazi kwa sasa. Kwa kufanya hivyo hakutaathiri vibaya fidia zao.
Katika barua pepe ndefu aliyowatumia wafanyakazi siku ya Alhamisi Mkurugenzi mkuu wa Airbnb ambaye pia ni muanzilishi mwenza Brian Chesky amewaeleza wafanyakazi sera mpya za kampuni hiyo na matarajio yao.
Chesky amesema kuwa mpango huo mpya utawafanya waweze kuajiri na kuhifadhi watu bora zaidi duniani tofauti na sasa ambapo wanalazimika kuwaajiri wale walio karibu tu na ofisi zao.
Kampuni hiyo ina wafanyakazi 6,000 dunia nzima , kati yao 3,000 wakiwa Marekani.