Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika yajipanga kuteka soko la almasi

B8936d03c13831bc0b27b995e193ef73 Afrika yajipanga kuteka soko la almasi

Sun, 31 Jul 2022 Chanzo: Habari Leo

Mawaziri wa madini kutoka nchi 19 barani Afrika zinazozalisha almasi (ADPA) wamepitisha Katiba ya Jumuiya hiyo yenye lengo la kushindana na soko la dunia katika biashara ya almasi.

Mbali na katiba, pia wamepitisha sheria na kanuni zenye kulinda rasilimali ya madini ya almasi katika nchi hizo.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Madini, Dk Doto Biteko mara baada ya kikao hicho cha dharura cha mawaziri wa nchi hizo na kusema kuwa katika kuimarisha ADPA wameamua kuajiri Mtendaji Mkuu na manaibu wawili ili waweze kuwajibika kwa umoja huo.

Biteko alisema maamuzi hayo yote yaliyofanywa na mawaziri wa ADPA kwa kiasi kikubwa yamelenga nchi husika kuwa na umoja wenye nguvu na kuwa na kauli ya pamoja yenye kuinua biashara ya almasi Afrika.

Alisema katika mkutano huo ambao Tanzania ni Mwenyekiti na mwenyeji, pamoja na mambo mengine imehakikisha kuwa umoja huo unakuwa na nguvu na kubadilisha baadhi ya sheria, kanuni na kuwa na katiba yenye nguvu kwa maslahi ya Afrika.

Chanzo: Habari Leo