Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afrika tumieni vyema soko la AfCFTA

Dkt Kijaji Awataka Wafanyabiashara Dodoma Kuchangamkia Fursa Afrika tumieni vyema soko la AfCFTA

Wed, 31 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji ambaye pia ni Mwenyekiti wa mkutano wa 13 wa Mawaziri wa Biashara kutoka nchi Wanachama wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Afika (AfCFTA), amezisisitiza nchi wanachama wa mkataba huo kutumia vema fursa zilizopo ili kukuza biashara.

Dkt. Kijaji ameyasema hayo Januari 30, 2024 alipokuwa akifungua mkutano wa 13 wa Mawaziri wa Biashara wa AfCFTA unaofanyika nchini Afrika Kusini.

Amezitaka nchi hizo kuendelea kushirikiana katika kukamilisha Itifaki ya Uwekezaji, Itifaki ya Biashara ya Kidigitali pamoja na majadiliano kwenye vigezo vya uasili wa bidhaa na kukamilisha masuala muhimu yanayohusu mifumo ya utatuzi wa migogoro katika ufanyaji biashara kupitia Mkataba wa Eneo Huru la Biashara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live