Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afisa Lishe awataka wanawake kujiingiza kilimo cha vanila

Afisa Lishe Awataka Wanawake Kujiingiza Kilimo Cha Vanila Afisa Lishe awataka wanawake kujiingiza kilimo cha vanila

Fri, 7 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Afisa Lishe katika Mradi wa Viungo Mkombozi Christopher amewataka Wanawake na Vijana kujiingiza katika kilimo hasa cha Vanila ili kujikwamua kiuchumi.

Ameyasema hayo huko Ofisi za Viungo Mwanakwereke Wilaya ya Magharib B wakati alipokua akitoa mafunzo maalum kwa wakulima walio chini ya mradi wa viungo kuhusiana na mbinu bora za kuhifadhia chakula.

Amesema kuwa iwapo watajishuhulisha na kilimo hicho kutawasaidia kupata mahitaji yao na kuwataka wakulima hao kulima hasa zao la Vanilla kwani ndio zao linalostahamili ukame.

Aidha amefahamisha kuwa mafunzo hayo ni ya awamu ya tatu kwa walimu wa Vikundi vya wakulima hao ambayo yanaelekeza jinsi ya kusarifu na kuhifadhi chakula ili kiweze kukaa kwa muda mrefu na salama kwa matumizi ya binadamu.

Ameeleza kuwa licha ya mafunzo hayo pia wakulima hao wamepatiwa vihifadhio vya mazao ikiwemo chupa za kigae 396 kwaajili ya kuhifadhia juisi ya nyanya, maboksi 1332 ya kuhifadhia mbogamboga (ZIPPERBAG) na Vipolo maalum vya kuhifadhia viungo (PADUU) 500.

Afisa ameongeza kwa kusema kuwa vifaa hivvyo watakabidhiwa wakulima 149 Unguja na wakulima 50 kwaupande wa Pemba ili kuhifadhia bidhaa zao na kuweza kuakaa kwa muda mrefu bila kuharibika.

Nao Wakulima wa Viungo kutoka Kizimbani na Donge Mbiji wamesema wamenufaika na mradi huo kutokana na elimu wanazopatiwa mara kwa mara kwani wameweza kujiamini na kuweza kulima mazao na kuyachakata wenyewe.

Aidha wamefahamisha kuwa licha ya elimu walioipata, mradi umewawezesha kulima kisasa kwa kuwapatia miundombinu mbakimbali ikiwemo maji na kusema kuwa vifaa walivyopatiwa katika kuhifadhia vitawasaisdia kuhifadhia bidhaa zao kwa matumizi ya baadae.

Hata hivyo wamewashauri wakulima wenzao kulima kilimo cha biashara kitakachowasaidia kutoka kimaisha.

Nae Mkulima wa Bustani za nyumbani( Kitchen Garden) kutoka Migombani Sharif Said Nambaga amewashauri wanawake na Vijana wasijiache kwa kutegemea ajira kutoka Serikalini na badala yake kujikita katika kilimo cha mbogamboga ikiwemo mchicha naTembere ili kujiongezea kipato.

Mafunzo hayo ya siku moja yametolewa na mradi wa viungo chini ya ufadhili wa umoja wa ulaya kupitia mradi wa Agri-Connect na kuwashirikisha wakulima wa viungo,matunda na mbogamboga kutoka Mjini na Vijijini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live