Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AfDB: Uchumi wa Afrika ulishuka 2023

Uchumi Kupanda AfDB: Uchumi wa Afrika ulishuka 2023

Mon, 19 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) imesema Ukuaji wa Uchumi wa Bara la Afrika kwa Mwaka 2023 ulishuka hadi kufikia 3.2% kutoka 4.1% ya Mwaka 2022

AfDB imefafanua kuwa hali hiyo imechangiwa na kutokuwa na utulivu wa Kisiasa kwenye baadhi ya Mataifa, Kudorora kwa Uchumi wa China, Athari za UVIKO-19 pamoja na Vita ya Urusi na Ukraine

Hata hivyo, Ukuaji wa jumla wa Pato la Taifa (GDP) kwa Bara la Afrika unatarajiwa kuwa kati ya wastani wa 3.8% Mwaka 2024 na 4.2% Mwaka 2025. Pia, Afrika inatazamiwa kuwa eneo la pili kwa ukuaji wa kasi wa Uchumi ikilifuatia Bara la Asia.

Nchi 3 za Afrika Mashariki zimetajwa katika orodha hiyo ambapo zitaongozwa na Rwanda inayotarajiwa kupata Ukuaji wa 7.2% ikifuatiwa na Tanzania 6.1% na Uganda itakayokua na Ukuaji wa Uchumia wa 6%.

Afrika itachangia uchumi wa nchi kumi na moja kati ya 20 zinazokuwa kwa kasi zaidi duniani mwaka 2024, Kundi la Benki ya Maendeleo ya Afrika lilisema katika Utendaji na Mtazamo wa Uchumi Mkuu (MEO) wa bara hilo iliyotolewa Ijumaa.

Kwa ujumla, ukuaji wa Pato la Taifa (GDP) kwa bara unatarajiwa kuwa wastani wa 3.8% na 4.2% mwaka 2024 na 2025, mtawalia. Hii ni ya juu zaidi kuliko makadirio ya wastani ya kimataifa ya 2.9% na 3.2%, ripoti ilisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live