Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AfDB: Tanzania kuzipita Kenya, Uganda kwenye uchumi

Wabunge EALA Wahadharisha Ubaguzi Uwekezaji Wa Bandari AfDB: Tanzania kuzipita Kenya, Uganda kwenye uchumi

Wed, 21 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uchumi wa Tanzania unatarajia kukua zaidi mwaka 2024 kupita uchumi wa Kenya na Uganda kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).

Katika ripoti mpya ya Utendaji na Matarajio ya Kiuchumi (MEO), AfDB inatabiri kuwa uchumi wa Tanzania utakua kwa asilimia 6.1, ukiwa mbele ya nchi za Afrika Mashariki (Uganda asilimua 6 na Kenya asilimia 5.4) isipokuwa Rwanda ambayo uchumi wake utakua kwa asilimia 7.2.

Tanzania pia inashika nafasi ya tisa kati ya nchi 11 za Afrika ambazo uchumi wake unatarajiwa kufanya vizuri nyuma ya Niger (asilimia 11.2), Senegal (asilimia 8.2), Libya (asilimia 7.9), Rwanda (asilimia 7.2), Côte d'Ivoire (asilimia 6.8), Ethiopia (asilimia 6.7), Benin (asilimia 6.4) na Djibouti (asilimia 6.2). Nchi zinazokamilisha orodha hiyo ni Togo na Uganda ambazo zinatarajiwa kukua kwa asilimia 6 kila moja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live