Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya eneo huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA) Dkt. Wamkele Mene amesema, wafanyabiashara wadogo na wale wa kati Barani Afrika wanakabiliwa na changamoto kadhaa kwenye kuendeleza biashara zao.
Dkt. Mene amesema kuwa kundi hilo linakabiliwa na ukosefu wa mitaji kutokana na taasisi nyingi za fedha kushindwa kutoa fedha kwa ajili ya mikopo ya biashara zao na hivyo kukosa mitaji ya kutosha.
Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa pili wa Wafanyabiashara wanawake Barani Afrika chini ya Mkataba wa eneo huru la biashara (AfCFTA) unaofanyika kwa mara pili hapa nchini.
Dkt. Mene amesema, AfCFTA inaendelea na mazungumzo na taasisi za fedha ikiwa ni pamoja na Mabenki kuweza kuwa na utaratibu wa kuwahudumia wafanyabishara wadogo na wale wa kati ili kuendeleza biashara zao.