Kampuni ya Adidas ipo hatarini kuzidiwa na wapinzani wao, Puma katika kutawala soko la biashara ya mchezo wa soka kutokana na kuelekea kupata hasara ya Pauni Milioni 450.
Adidas inatarajiwa kupata hasara hiyo kubwa kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 30 kutokana na kutouza mzigo wa bidhaa walizoshirikiana na mwanamuziki Kanye West, ikielezwa kuwa bidhaa zilizobaki ndani aina ya 'Yeezy' zina thamani ya Pauni Bilioni 1.1.
Baadhi ya wachezaji wenye majina makubwa wanaovaa viatu vya Adidas ni Lionel Messi, Mohamed Salah na Paul Pogba, pia wanamkataba wa kuuza vifaa na jezi za Manchester United wenye thamani ya Pauni Milioni 750.
Puma hivi karibuni waliingia mkataba na Jack Grealish, pia wana mkataba na Neymar na Klabu ya Manchester City.