Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Acacia yatoa Sh80 milioni rambirambi MV Nyerere

20087 Pic+accasia TanzaniaWeb

Mon, 1 Oct 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kampuni ya uchimbaji dhahabu ya Acacia imetoa mkono wa pole wa Sh80 milioni kwa waathirika wa ajali ya MV Nyerere.

Kivuko cha Mv Nyerere kilipinduka Septemba 20, 2018 katika kisiwa cha Ukawa, wilayani Ukerewe jijini Mwanza na kusababisha vifo vya watu 230 na manusura 41.

Licha ya fedha hizo zilizokabidhiwa serikalini, kampuni hiyo ilituma wataalamu wake kusaidia uokozi na kutoa huduma nyingine muhimu kwa walionusurika pamoja na waliopoteza maisha.

Taarifa ya jana Septemba 29, 2018 iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Acacia, Asa Mwaipopo imeeleza kuwa fedha hizo zitasaidia kuzifuta machozi familia zilizoathirika na ajali hiyo.

“Tunaziombea familia zilizoathirika. Tunaipongeza timu ya uokoaji iliyofanikisha kuwanusuru majeruhi 41 kwenye ajali hiyo. Tumejitoa kadri tuwezavyo,” amesema Mwaipopo

Chanzo: mwananchi.co.tz