Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Abu Dhabi kumwaga wawekezaji hoteli Z’bar

00bc8c7f0efc3685dd9ec7ad20d2014c Dkt Mwinyi akiwa na ugeni toka Abudhabi

Tue, 29 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi amekutana na uongozi wa Kampuni ya International Holding Company (IHC) ya Abu Dhabi, na kuwaeleza fursa zilizoko katika uchumi wa bluu.

Kampuni hiyo ni kubwa katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na ya pili kwa nchi za Magharibi ambako katika mkutano huo wa Abudhabi imeahidi kuleta wawekezaji wa kigeni Zanzibar kwa ajili ya kuwekeza katika miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa hoteli za kitalii.

Rais Mwinyi katika mazungumzo hayo aliwaeleza kwa undani wawekezaji hao wa IHC fursa zilizomo katika uchumi wa bluu na kuwaalika kuja Zanzibar ambapo mazingira ya uwekezaji yameimarishwa.

Alisema Zanzibar kwa sasa inahitaji wawekezaji makini huku akieleza kwamba moja ya fursa zilizomo katika uchumi wa bluu ni uwekezaji katika visiwa vidogo vidogo vinavyofikia 53 katika bahari ya Zanzibar.

Fursa nyingine zinazoambatana na uwekezaji wa uchumi wa bluu alizozieleza Rais Mwinyi ni uchimbaji wa mafuta na gesi asilia, uvuvi mkubwa katika bahari kuu, ujenzi na kuzifanyia matengenezo meli za uvuvi, ujenzi wa bandari kubwa zitakazoweza kuhimili meli kubwa za mizigo ambako maeneo yametengwa ya Mangapwani na Mpigaduri Unguja.

Aidha, Rais Mwinyi amesisitiza kwamba yote hayo yatafanikiwa iwapo kutakuwa na miundombinu mizuri katika huduma za kijamii na kuwaeleza wawekezaji hao umuhimu wa kusaidia huduma za kijamii za elimu na afya na kuanzisha mikakati maalumu ya kiuchumi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA), Shariff Ali Shariff akitoa mwelekeo wa fursa za uwekezaji kwa wawekezaji hao, aligusia hali ya watalii ilivyo Zanzibar ambako licha ya ugonjwa wa Covid-19, ambako alisema Zanzibar inaendelea na kupokea watalii 39,512 kati ya Januari hadi Desemba mwaka jana.

Alieleza kuwepo kwa fursa za kuwekeza katika kuchakata bidhaa za baharini, ujenzi wa boti za uvuvi na kuzifanyia matengenezo, ujenzi wa mji mwingine utakaoitwa Zanzibar Marina City na kusaidia kilimo cha mwani ambacho kinalimwa na idadi kubwa ya wanawake.

Sharif alieleza haja kwa wawekezaji hao kuisaidia Zanzibar kuwa na kituo cha kukuza vipaji kwa michezo mbalimbali hali itakayoipaisha Zanzibar katika sekta ya michezo.

Mkurugenzi huyo alibainisha kuwepo kwa hekta 6,000 za ardhi inayohitaji kuendelezwa eneo la Makurunge, ardhi ambayo ni mali ya Zanzibar na inafaa kwa ajili ya kilimo cha aina mbalimbaliikiwemo miwa.

Katika hatua nyingine, Rais Mwinyi amekutana na Waziri wa Nchi anayeshughulikia Mambo ya Nje, Shehe Shajkboot Nahyan Al Nahyan na kuzungumzia uhusiano baina ya Tanzania na UAE, ambako pamoja na mambo mengine alizungumzia ufunguzi wa Ubalozi Mdogo waUAE Zanzibar na kurejesha huduma za ndege za UAE Zanzibar.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live