Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Abiria wapungua Ubungo

33192 Pic+ubungo Kituo cha mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam

Mon, 24 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Baada ya Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa majini na nchi kavu (Sumatra) kuruhusu mabasi ya kati (abiria 28) abiria wamepungua katika Kituo cha mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.

Sumatra waliruhusu magari hayo jana Jumapili baada ya kuwapo kwa msongamanao wa abiria kituoni hapo na kukosa usafiri.

Akizungumza leo Desemba 24,2018, Mkurugenzi wa udhibiti wa barabara kutoka Sumatra, Johansen Kahatano amesema waliamua kuchukua uamuzi huo jana baada ya abiria kulundikana kituoni hapo.

"Jana tuliruhusu coaster zibebe abiria baada ya magari tuliokuwa tunayaruhusu kuisha ambapo zilitusaidia sana kupunguza msongamano" amesema Kahatano.

Amesema abiria waliokuwa wanaenda mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha wamepungua waliobaki ni wa Morogoro na Dodoma.

"Tunafanya utaratibu kama wajana kuhakikisha abiria wa Morogoro na Dodoma wanasafiri ikiwa ni pamoja na kuruhusu magari kwenda na kurudi" amesema.

Hata hivyo, abiria wamelalamikia kutozwa nauli kubwa na magari hayo kwa madai yakienda yanarudi bila abiria.

Abiria wanaokwenda Moshi wamekuwa wakitozwa Sh30,000 badala ya Sh28,000 wakati na Arusha Sh35,000 badala ya Sh32,000.

Filbert Lizer amesema amelipa bei hiyo kwenda Arusha kutokana na shida ya usafiri lakini hiyo sio nauli ya kawaida.

"Kwakuwa tuna shida ya usafiri lakini bei ya kawaida huwa tunalipa Sh32,000 tutafanyaje wakati magari hakuna?" amehoji Lizer

Abiria mwingine Mwamini Faiz amesema yeye anakwenda Lushoto lakini nauli aliyolipa ni Sh25,000 badala ya Sh20,000

Mwenyekiti wa Chama cha Kutetea Abiria (Chakua) Hassan Mchanjanjama amesema kupanda kwa nauli kunatokana na gharama za kufunga kifaa cha kufuatilia mwenendo wa gari.

Amesema kila anaenda kuomba kibali anapaswa kulipa Sh180,000 kwaajili ya kufunga kifaa hicho .



Chanzo: mwananchi.co.tz