Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Abiria Ubungo wasotea usafiri, Latra wataja sababu

89548 Abiria+pic Abiria Ubungo wasotea usafiri, Latra wataja sababu

Mon, 23 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Licha ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (Latra) kuruhusu magari madogo ya abiria aina ya Coaster kubeba abiria kutoka Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam kwenda mikoani, hali ya usafiri kituoni hapo si nzuri.

Leo Jumapili Desemba 22, 2019 Mwananchi limeshuhudia abiria wakiwa wamekata tamaa kutokana na kukosa usafiri, huku wengine wakidai wanasubiri mabasi yatakayofika mchana.

Sophia Michael amesema, “Mimi nakwenda Tanga na sikujua kama nitakutana na tatizo la usafiri. Nilisikia kuna magari yameruhusiwa kubeba abiria lakini nimekuta hali tofauti.”

"Nilijua uwepo wa treni ya Dar es Salaam Moshi nayo itaokoa jahazi kumbe ni tofauti.”

Naye Mwasiti Ramadhani msafiri kwenda mkoani Morogoro amesema wameambiwa wasubiri hadi mchana gari zitakuwepo.

"Tunasubiri basi la kampuni ya Abood lililoondoka asubuhi lirudi ila hali ya usafiri ni mbaya nikisema nirudi nyumbani kesho ndio hali itakuwa mbaya zaidi,” amesema Mwasiti.

Ofisa leseni wa Latra,  Leo Ngowi amesema vibali vilivyotolewa  vinatosha ila tatizo ni wanaotakiwa kukata vibali kushindwa kukamilisha taratibu.

"Tuna uhakika vibali tulivyotoa vitatosha kusafirisha abiria wote tatizo wamiliki hawakamilishi masharti tuliyotoa na kuchelewa kunasababisha kuchelewa kwa ufungaji wa vidhibiti mwendo,” amesema Ngowi.

Amesema kwa abiria wa Dodoma na Morogoro wao wanasubiri magari yaliyoondoka alfajiri ambayo yameruhusiwa kurudi Dar es Salaam na kuchukua abiria wengine.

Chanzo: mwananchi.co.tz