Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Abiria Fastjet wasubiri nauli hadi jioni

32721 Pic+fastjetTanzania Web Photo

Fri, 21 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Katika kutekeleza maelekezo ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Shirika la Ndege la Fastjet limeanza kurejesha nauli za abiria waliokata tiketi, lakini hadi jana jioni abiria walikuwa hawajaanza kulipwa.

Baada ya tamko la TCCA mwanzoni mwa wiki kuitaka Fastjet kulipa madeni ya watoa huduma wake yanayofika Sh1.4 bilioni, ilitangaza kurudisha nauli za abiria waliokuwa wamekata tiketi.

Akizungumza na Mwananchi jana, meneja mawasiliano wa shirika hilo, Lucy Mbogolo alisema wametenga fedha za kutosha na wataanza kuwalipa abiria waliokata tiketi kwa kulipa fedha taslimu.

“Wanachotakiwa (abiria) kufanya ni kwenda kwenye ofisi zetu na kuonyesha tiketi zao. Wale waliolipia kwa simu za mkononi au kupitia akaunti ya NMB watarejeshewa kwenye akaunti zao,” alisema.

Hata hivyo, Mwananchi lilifika katika ofisi za Fastjet jijini Dar es Salaam na kuzungumza na baadhi ya abiria waliokuwa wakisubiri kurejeshewa fedha ambao walionyesha wasiwasi kuzipata.

Mmoja wa abiria aliyejitambulisha kwa jina la John Peter alisema, “Tunasubiri kurejeshewa fedha, lakini tumeambiwa viongozi wako kwenye kikao huko ndani na ni muda mrefu umepita tunasubiri.”

Hadi saa 11 jioni Mwananchi lilipoondoka katika ofisi hizo malipo yalikuwa bado hayajatolewa.



Chanzo: mwananchi.co.tz