Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ATM za kununua taulo za kike yabuniwa Tanzania

64877 Atm+pic

Sat, 29 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Adha ya kukatisha masomo kwa wanafunzi wa kike wawapo katika siku zao ‘hedhi’ huenda ukawa historia baada ya wabunifu kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph kubuni mashine ya ATM kwa ajili ya taulo za kike.

Tofauti na ATM ya kutolea fedha mashine hii ambayo huwekwa katika vyoo vya shule ina mfumo maalumu ambapo mwanafunzi atalazimika kutumia kadi yake kitoa taulo pindi anapopata dharura akiwa katika masomo.

Akizungumza leo Jumamosi Juni 29 2019 katika maonyesho 43 ya biashara ya kimataifa ya sabasaba jijini Dar es Salaam nchini Tanzania, David Msemwa mwanafunzi wa shahada ya mawasiliano na elektroni amesema mashine hiyo ambayo huwekwa inaweza kutumika pia katika ofisi mbalimbali za umma na binafsi.

Amesema baada ya kufanya utafiti wamegundua wanafunzi wa kike wanakosa vipindi mara baada ya kuingia kwenye siku zao ambapo watalazimika kurudi nyumbani huku wakiwa wamepitwa na takribani vipindi vitatu hadi vinne.

“Mwanafunzi atatakiwa kuwa na kadi yake ambayo imeunganishwa kwenye mfumo wa malipo, tofauti na ile ya kutolea pesa hii huwa huingizwa ndani ya mashine bali atapangusa kisha pakiti ya pedi itatoka kama zitokavyo Pesa,” amesema msomi huyo.

Ameongeza  mwanafunzi atakatwa kiasi cha Sh2000 (itategemea na bei elekezi) lakini pia kama mwanafunzi kadi yake itaishiwa pesa kuna sehemu ambayo atatakiwa kuingiza Sh 500 na atapata taulo moja ambalo litamsaidia kwa masaa machache.

Pia Soma

“Malipo yake ni kama ilivyo kadi za mabasi ya mwendokasi ambapo mzazi ataingiza salio aidha la mwezi au zaidi na litakapoisha atajulishwa na uongozi wa shule ili aweze kulipia tena,” amesema.

Mbali na hilo Msemwa ambaye alishirikiana na wanafunzi wenzake wawili amesema suala la taulo za kike bado ni changamoto hivyo ameiomba Serikali kulifuatilia suala hili kwa umakini ili wanafunzi wasome siku nzima bila kukatisha masomo yao.

“Lakini pia Serikali inaweza kuua ubunifu huu kama sehemu ya utatuzi kwani endapo kila shule zitafungwa mashine za taulo za kike katika vyoo vyote vya shule za Msingi na sekondari na wakaweka kima cha chini cha bei kuwa ni 1000 haya malumbano ya kila siku kuhusu taulo za kike yatakwisha,” amesema

 

Chanzo: mwananchi.co.tz