Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ATE walalamikia mrundikano wa kodi

Ate Pic Data Jane Nyimbo akizungumza kwenye maadhimisho ya Mei Mosi

Mon, 2 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha Waajiri Nchini (ATE) kimelalamikia mlundikano wa kodi zinazotozwa nchini wakisema zimeongeza gharama kwa waajiri.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa ATE, Jane Nyimbo leo Jumapili, Mei Mosi 2022, katika sherehe za siku ya wafanyakazi duniani zinazofanyika katika uwanja wa Jamuhuri jijini hapa.

“Waajiri wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo mlundikano wa kodi ambazo wamekuwa wakitozwa na mamlaka mbalimbali na hali hiyo inaongeza gharama ya kufanya biashara kutokana na ugumu katika mazingira ya biashara,” amesema.

Amesema changamoto hiyo imewafanya baadhi ya waajiri kulazimika kupunguza wafanyakazi hasa katika sekta ambazo zimeathiriwa na janga la ugonjwa wa Ukimwi na Uviko-19.

Ametoa mfano wa sekta hizo ni ya ukarimu na utalii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live