Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ATCL yasitisha safari zote za ndege nje ya Tanzania

100054 Pic+atcl ATCL yasitisha safari zote za ndege nje ya Tanzania

Thu, 26 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Shirika la Ndege Tanzania (ATCL)  kuanzia Machi 25, 2020 litasitisha safari zake za nje ya Tanzania ikiwa ni  sehemu ya kukabiliana na virusi vya corona.

Kwa mujibu wa taarifa ya ATCL iliyotolewa leo Jumatatu Machi 23, 2020 inaeleza kuwa safari hizo ni  Entebe(Uganda), Bujumbura(Burundi), Hahaya(Comoro), Lusaka(Zambia) na Harare (Zimbabwe).

Kampuni hiyo imesema haitarejesha fedha  badala yake abiria wote wenye tiketi katika safari zilizositishwa wanatakiwa kuwasiliana na ofisi za kampuni hiyo au wakala wa safari za ndege kwa ajili ya taratibu za kubadilisha tiketi hizo ili zitumike  baadaye katika safari zao bila makato.

“Tumesitisha kwa sababu ya matamko na maagizo ya serikali mbalimbali katika nchi tunazofanya safari zetu, matamko hayo ni kufunga mipaka na kupunguza mwingiliano kwa sababu ya corona,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa ACTL, Ladislaus Matindi.

 

“Tutarudisha safari hizo hali itakapoturuhusu. ATCL itaendelea kutoa huduma za ndani japo kwa kupunguza miruko katika baadhi ya vituo kutokana na upungufu wa abiria kipindi hiki cha tahadhali  nyingi.”

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
Matindi ameahidi kampuni hiyo kuendelea kujali usalama na afya za wafanyakazi, abiria na wateja kwa kupuliza dawa, kusafisha kwa dawa maalumu ndani ya ndege na mikono.

Chanzo: mwananchi.co.tz