Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ATCL yapunguza hasara takriban asilimia 50-Ripoti

51630 ATCL+PIC

Thu, 11 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imebainisha kuwa mashirika 14 ya umma yana matatizo ya kifedha na kupata hasara hadi kusababisha madeni zaidi ya mitaji yao kwa zaidi ya asilimia 100.

Hata hivyo, CAG amesema hasara kwa ATCL imepungua kwa asilimia 58 kutoka Sh38.72 bilioni mwaka 2005/6 mpaka Sh16.21 bilioni mwaka 2016/17.

“Hasara imepunguza mtaji wa kampuni mpaka kufikia mtaji hasi. Kwenye miaka mitatu ya karibuni nimeanza kuona mwenendo mzuri wa kampuni maana hasara imepungua kutoka Sh38.72 bilioni ya mwaka 2005/06 mpaka Sh16.21 bilioni mwaka 2016/17, kupungua kwa takribani asilimia 58,” imebainisha ripoti hiyo.

CAG amefafanua kupungua kwa hasara kumetokana na kuongezeka mapato kwa asilimia 20 na kupungua gharama za uendeshaji kwa asilimia 27.

Katika kipindi hicho, ATCL ilikodishwa na Serikali ndege mbili aina ya Bombardier ambazo zilirejesha huduma za usafiri wa anga ambazo zilikuwa zinasuasua. Hadi sasa ATCL ina ndege imekodishwa ndege sita--bombardier tatu, Airbus mbili na Dreamliner moja-- ambazo zinafanya safari za ndani na nje.

Ripoti hiyo pia inaonyesha kuwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inadai jumla Sh1.46 trilioni kwa wahitimu waliokopa, lakini imeshindwa kuwapata husika.

Amesema hali hiyo inapunguza uwezo wa bodi kuendelea kutoa mikopo kwa wanafunzi wapya na wanaoendelea.

Kuhusu Kampuni ya Mawasiliano ya Simu Tanzania (TTCL), CAG amegundua tofauti ya Sh24.71 bilioni kati ya taarifa zilizopo kwenye vitabu vya TTCL na taarifa zilizothibitishwa na wateja.

Amesema wateja walithibitisha jumla ya Sh100.46. bilioni wakati taarifa zilizopo kwenye vitabu zinaonyesha kuna deni la Sh125.18 bilioni.

CAG amesema TTCL haioanishi kila mwezi nyaraka walizonazo na zile za uthibitisho kutoka kwa wateja kwa ajili ya kupata usahihi.

Ripoti pia inasema kati ya mashirika 14 yanayojiendesha kwa hasara, mashirika 11 yana ukwasi hasi.

Taasisi hizo ni Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Lindi), Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), Bodi ya Utalii Tanzania, Shirika la Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam(Dawasco), Kampuni ya Maendeleo ya Nishati ya Joto Tanzania (TGDC).

Nyngine ni Baraza la Taifa la Biashara, Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (Mwanza), Kampuni ya Usafirishaji na Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usambazaji Umeme. Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa).



Chanzo: mwananchi.co.tz