Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ATCL yapata hasara ya 60 bilioni

Bd3511aa509f7e4f3b15116be33176de ATCL yapata hasara ya 60 bilioni

Sun, 28 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu Serikali, Charles Kichere amesema Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) limetengeneza hasara ya Shilingi bilioni 60 kwa mwaka na kwa kipindi chote cha miaka ya nyuma shirika hilo limekuwa likijiendesha kwa hasara.

CAG, Kichere amebainisha hayo wakati wa uwasilishaji wa ripoti yake kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kwa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma hii leo.

“Katika ukaguzi wetu wa mwaka 2019/2020 tumegundua Shirika letu la Ndege limetengeneza hasara mwaka huu ya Tsh bilioni 60 ila kwa miaka mitano pia limekuwa likitengeneza hasara, kuna changamoto ambazo Serikali inabidi iziangalie ili Shirika letu litekeleze majukumu yake vizur,”alisema Kichere.

Katika ripoti yake, CAG amesema amebaini Shirika la Ndege la ATCL limetengeneza hasara ya Shilingi bilioni 60 Kwa miaka mitano iliyopita na kudai kuwa shirika hilo limekuwa likijiendesha kwa hasara.

“Katika ukaguzi wetu wa 2019/2020 tumebaini ATCL imetengeneza hasara ya Tsh bilioni 60. Kwa miaka mitano iliyopita shirika limekuwa likitengeneza hasara,”alisema Kichere.

Chanzo: www.habarileo.co.tz