Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ATCL yaongeza safari za Dar- Dodoma

47340 ATCL+pic

Tue, 19 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) limeongeza safari zake kwa mkoa wa Dodoma ambapo sasa itakuwa ni kila siku wakati Jumatatu, Jumatano na Ijumaa itakuwa mara mbili kwa siku.

Mkurugenzi wa ATLC, Ladislaus Matindi amesema hayo leo Jumatatu Machi 18, 2019 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuwa uamuzi huo unatokana na mahitaji makubwa ya watu kwenda na kutoka Jijini Dodoma.

Matindi amesema Jiji la Dodoma sasa lina mahitaji mengi ya kiserikali hivyo wananchi kuwa na mahitaji ya kuja na kutoka.

Kiongozi huyo amesema hadi sasa ATCL imejiimarisha kikamilifu na kuwa na mawakala sehemu mbalimbali duniani na wanaendelea kufanya mawasiliano na mataifa na mashirika mengine ili kujiimarisha.

"Tumeshazungumza na mashirika na mataifa tofauti duniani ambako sasa tutaanza kurusha ndege zetu huko, lakini kikubwa tutaanza kurusha ndege kutokea Mwanza kwenda Ulaya," amesema.

Mwenyekiti wa bodi ya ATCL, Emmanuel Korosso ameiomba Serikali kutupia macho katika viwanja vya ndege vya Dodoma na Songwe ili kuruhusu ndege zitue hata nyakati za usiku.



Chanzo: mwananchi.co.tz