Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ATCL yajitetea kuahirisha safari mara kwa mara

63591 Atclpic.png

Thu, 20 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakati malalamiko ya abiria wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) yakiongezeka, uongozi wa shirika hilo umewaomba kutoa mawasiliano yao ya uhakika ili liwajulishe mapema endapo kutakuwa na mabadiliko yoyote.

Ufafanuzi huo umetolewa leo Juni 20, 2019 na mkurugenzi mkuu wa ATCL, Ladslaus Matindi alipozungumza na gazeti kuhusu malalamiko ya aliyekuwa mbunge wa Rungwe mpaka mwaka 2015 na waziri kwa nyakati tofauti, Profesa Mark Mwandosya.

Kwenye ukurasa wake wa Twitter (@MarkMwandosya) profesa huyo amelalamika kucheleweshwa kwa ndege yake aliyoapaswa kusafiri nayo Mei 29 kutoka Dar es Salaam kwenda Entebbe nchini Uganda.

Licha ya kufika kwa zaidi ya wakati unaoshauriwa, amesema ndege yake iliyokuwa iondoke saa 4:30 asubuhi iliahirishwa mpaka saa 9:00 alasiri. Profesa Mwandosya alifika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 1:00 asubuhi.

Juzi, Juni 18, ilikuwa asafiri saa 4:20 asubuhi kutoka Dar es Salaam kwenda Mbeya na akafika JNIA saa 1:15 lakini akajulishwa kuwa ndege ilishaondoka saa 1:00 asubuhi, robo saa iliyopita.

“Huu ni utaratibu mpya au ni kukosa ushindani?” amehoji Profesa Mwandosya.  

Pia Soma

Kwa utaratibu hasa wa safari za kimataifa, abiria anapaswa kufika uwanja wa ndege saa tatu kabla ya muda wa kuondoka.

Akijibu tuhuma za Mwandosya na abiria wengine wa shirika hilo waliokutwa na maswahibu tofauti, mkurugenzi mkuu wa ATCL, Matindi amesema ni kawaida kuwa na mabadiliko kwenye usafiri wa anga ingawa shirika husika hutakiwa kubeba dhamana ya usumbufu utakaojitokeza.

“Tunawaomba abiria wetu waandike namba za simu anazotumia ili kukiwa na mabadiliko tuwajulishe kwa wakati. Kinachotokea, tunapowatafuta huwa hatuwapati hivyo kuwa changamoto kwetu,” amesema Matindi.

Matindi amesema huwa wanajitahidi kuwatafuta abiria wao ili wawajulishe mawasiliano hayakamiliki kutokana na namba zao kutopatikana.

Chanzo: mwananchi.co.tz