Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ATCL yaimwaga rasmi NAS Airco, Swissport yapewa majukumu

90640 Atcl+pic ATCL yaimwaga rasmi NAS Airco, Swissport yapewa majukumu

Thu, 2 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar/Moshi. Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) imevunja mkataba wake na kampuni ya NAS-DAR Airco Company Limited sababu ikitajwa ni upungufu wa kiutendaji wa kampuni hiyo.

Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Januari 2, 2020 Mtedaji mkuu wa ATCL, Ladslaus Matindi amesema tayari kampuni yake imeingia mkataba na kampuni ya Swissport kufanya kazi hizo badala ya NAS- DAR Airco.

“Ni kweli tumewachukua Swissport, lengo ni kuboresha huduma kwa ajili ya kuwafurahisha wateja wetu,” amesema Matindi.

Alipoulizwa kuhusu mpango wa kuwa na kampuni yake binafsi ya kuzihudumia ndege za kampuni hiyo, Matindi amesema, “huo mpango uko pale pale miaka miwili mitatu ijayo.”

Kuvunjwa kwa mkataba huo kumekuja wakati ATCL ikiwa katika mkakati wa kuwa na kampuni yake binafsi itakayohudumia ndege zake ifikapo mwaka 2022.

Tayari kampuni ya Swissport imeanza kazi leo Alhamisi katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

Maokezi ya ndege ya ATCL katika uwanja wa ndege KIA ambao abiria waliokuwa wakipanda ndege hiyo pamoja na wafanyakazi wa Swissport walionekana wakishangilia ndege hiyo ilivyotua huku wakipeperusha vibendera vilivyoandikwa jina la Swissport.

Akizungumza na waandishi wa habari, katika hafla fupi iliyoandaliwa na Swissport kwa ajali ya kuipokea ndege hiyo uwanja wa ndege KIA, meneja wa Kanda ya Kaskazini wa ATCL, Estermerry Karumbo alisema wameamua kuungana na kampuni ya Swissport  kutokana na huduma zake ni nzuri.

“Leo tunafurahia kuungana na Swissport kufanya nao bishara pamoja kwa ajili ya kuboresha huduma zetu kwa Watanzania na kazi kubwa ya Swissport ni kusimamia utendaji mzima wa ndege, hivyo tutafanya nao kazi bega kwa bega na tuna imani nao na tunaamini tutafika nao sehemu ambayo tunatakiwa kufika,” alisema Karumbo

 

Chanzo: mwananchi.co.tz