Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ATCL watakiwa kuweka mikakati kujiendesha kwa tija

ATCL Kupunguza Safari Za Ndege ATCL watakiwa kuweka mikakati kujiendesha kwa tija

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

SERIKALI imelitaka Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kuhakikisha linapanga mikakati madhubuti itakayoliwezewesha kukua na kujiendesha kwa tija, baada ya uwekezaji mkubwa unaofanywa kupitia ununuzi wa ndege za masafa mafupi, ya kati na marefu.

Akizungumza wakati akifungua Kikao cha Tano cha Baraza la Pili la Wafanyakazi mkoani Morogoro, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Uchukuzi, Lucas Kambelenje ambaye amemuwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, amesema ununuzi wa ndege hizo unaofanywa pamoja na maboresho katika viwanja unatarajiwa kuongeza tija katika usafiri wa anga nchini.

“Kama serikali tunategemea ndege hizi 14 zilizonunuliwa ziwe na matokeo chanya ambayo yataonekana na niwahakikishie kuwa ndege zilizobaki serikali itahakikisha zinakuja, ili shirika liendelee kupiga hatua,” amesema Kambelenje.

Ameipongeza ATCL kwa kuhakikisha inapunguza gharama za uendeshaji kwa kuwawezesha wataalam wao kufanya matengenezo ya ndege wenyewe, ili kupunguza utegemezi wa kampuni za nje hadi kiwango cha matengenezo makubwa (C Check) hapa nchini na hivyo kuokoa kiasi kikubwa cha fedha, ambazo zingelipwa kwa kampuni za nje ya nchi,

Ameitaka ATCL kuhakikisha inaboresha huduma kwa wateja ili kuvutia wateja wengi zaidi kutumia Shirika hilo kwa safari za ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa baraza hilo, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi, amesema ATCL imeweza kuweka mifumo mbalimbali inayowezesha mauzo kufanyika vizuri pamoja kuingia makubaliano na mashirika mengine ya kimataifa, ili kupata wateja kwenye maeneo ambayo ATCL haitoi huduma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live