Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ATCL watakiwa kutazama upya gharama za tiketi

8d113e68a368df879a17324836f2e335 ATCL watakiwa kutazama upya gharama za tiketi

Thu, 18 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri wa Uchukuzi, Atupele Mwakibete, ameitaka Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) kutazama upya gharama za tiketi zilizopangwa kwenye ndege zao, kwenda maeneo mbalimbali nchini, ili kuvutia wateja wengi zaidi kutumia shirika hilo.

Akizungumza mkoani Katavi, wakati alipotembelea Kiwanja cha Ndege cha Mpanda, Naibu Waziri Mwakibete amesemaa uwepo wa gharama kubwa za tiketi, unachangia uchache wa abiria wanaotumia shirika hilo, japo takwimu zinaonesha ongezeko la abiria kwa safari za ndani kupitia kiwanja hicho .

“Takwimu nilizosomewa hapa zinaonesha ongezeko la abiria na safari za ndege, lakini naambiwa hapa abiria bado wapo wa kutosha, lakini wanakwazwa na gharama za nauli, mkiangalia upya nina imani zinaweza kushuka kidogo na kuwezesha abiria wengi zaidi kutumia ndege zetu," alisema Naibu Waziri Mwakibete.

Mwakibete amesema serikali imeichukua changamoto ya udogo wa jengo la abiria kiwanjani hapo na kuahidi kuwa itatafuta fedha ili kujenga jengo litakaloendana na hadhi ya kiwanja hicho.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuf ameishukuru serikali kwa kuhakikisha ATCL inaongeza safari zake mkoani humo, kutoka safari moja kwa wiki mpaka kufikia safari nne kwa wiki, uamuzi uliorahisisha shughuli za kibiashara baina ya mkoa huo na mikoa mingine.

Kwa upande wake Meneja wa Uwanja wa Ndege Mpanda Jeff Shantiwa, amesema TAA inaendelea kuhakikisha kiwanja hicho kinatoa huduma stahiki kulingana na kanuni na taratibu za usafiri wa anga duniani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live