Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ATCL kuzindua safari ya Mumbai leo

67105 Pic+atcl

Wed, 17 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) leo Jumatano litazindua safari yake ya saba ya kimataifa kuelekea Mumbai nchini India baada ya uzinduzi wa ile ya kuelekea baada ya kuzindua ile ya Johannesburg mwezi uliopita.

Safari hiyo ya kwanza ya kuelekea Mumbai itafanyika saa moja na nusu jioni ya leo Julai 17 mwaka 2019, Safari tatu zitakuwa zikifanyika kwa wiki na nauli kwa sasa ni Dola za Kimarekani 378 sawa na Sh869,362 kwa tiketi ya kwenda na kurudi.

Juni 28, 2019 shirika hilo ambalo lilifufuliwa upya na Serikali mwaka 2016, lilifanya safari yake ya kwenda Johannesburg nchini Afrika Kusini huku safari hiyo ikitajwa kuvunja rekodi ya kuwa safari ya kwanza ya kimataifa ya shirika hilo iliyokuwa na abiria wengi kwa siku ya kwanza.

Safari ya Mumbai inatajwa kuwa iliitikiwa vyema kwa abiria wengi kukata tiketi lakini bado haijafahamika kama itavunja rekodi hiyo ya Afrika Kusini.

Aidha kuzinduliwa kwa safari hiyo leo Jumatano kunaiongeza India katika orodha ya nchini ambazo ATCL inafanya safari zake, hivi sasa inatua Comoro, Burundi, Uganda, Zambia, Zimbabwe na Afrika Kusini.

ATCL lenye marubani 70 lina jumla ya ndege nane zinazofanya kazi, tatu zikiwa aina ya Bomberdier Q400, Airbus A220 – 300 mbili , Fokker 50 moja, Foker 28 moja na  Boeing 787 – 8 (Dreamliner) moja, aidha ndege moja aina ya Bomberdier Q300 ni mbovu.

Pia Soma

Nchini Tanzania shirika hilo linafanya safari kati ya mikoa ya Dar es Salaam na Bukoba, Dodoma, Kigoma, Kilimanjaro, Mtwara, Mbeya, Mwanza, Songea, Tabora, Iringa na Zanzibar.

Chanzo: mwananchi.co.tz