Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ATCL kushusha chuma kingine mwezi huu

Atcl Pic Data ATCL kushusha chuma kingine mwezi huu

Mon, 6 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali imesema Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), linatarajiwa kuingiza ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner mwishoni mwa mwezi huu.

Mkakati huo wa Serikali unalenga kuliongezea nguvu shirika hilo ili kujiendesha kwa ufanisi na kuendelea kumiliki soko la ndani na nje ya Tanzania. Hayo yameelezwa leo Jumatatu, Mei 6,2024 na Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, wakati akiwasilisha makadirio na mapato na matumizi ya wizara bungeni, Dodoma.

Amesema kuwasili kwa ndege hiyo hiyo kutalifanya shirika kuwa na jumla ya ndege 16 ikiwemo Boeing 737-9 Max iliyowasili nchini Machi, 2024.

“Ndege hizo zitasaidia ATCL kuendelea kupanua mtandao wake wa safari za ndani na nje ya nchi ili kuchochea ukuaji wa sekta nyingine za uchumi kama utalii, madini, biashara, kilimo, mifugo na uvuvi,” amesema Profesa Mbarawa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live