Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ATCL kusafiri Afrika Kusini kwa bei ya punguzo

62754 ATCL+PIC

Sat, 15 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Likitarajia kuanza kurukwa kwenda Johannesburg, Afrika Kusini, Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) limetoa tiketi kwa watu watatu walioibuka washindi kwa kujibu maswali yaliyoulizwa kwenye mitandao ya kijamii.

Meneja masoko wa ATCL, Christina Tungaraza amesema shindano hilo lilifanyika kuanza mwezi Mei na kuhitimishwa Juni 13.

"Lengo lilikuwa kutangaza bei ya punguzo ya safari za kwenda Johannesburg ambayo ni Dola 299 za Marekani kwenda na kurudi," amesema.

Baada ya kuisha kwa promosheni hiyo itakayokamilika Julai 15, amesema nauli itakuwa ni Dola 347. Amewahamasisha Watanzania na wafanyabiashara kutumia fursa hiyo kusafiri na ATCL kwa bei ya punguzo.

Washindi waliojipatia tiketi hizo kuzindua safari za ATCL kwenda Afrika Kusini kwa mara kwanza ni Augustine Rutasingwa, Habibi Luzinga na Jeff Nzigo ambao watasafiri Juni 28, safari hizo zitakapoanza.

Ili kushinda tiketi ya bure, Tungazara amesema washiriki walitakiwa kujibu maswali yaliyokuwa yakiulizwa.

Pia Soma

Mmoja wa washindi hao, Habibu Luzinga ambaye ni mwanafunzi wa udaktari amesema ni mara yake ya kwanza kwenda Afrika Kusini.

"Nilikuwa na ndoto ya kwenda nje ya nchi ila sikujua kama itakuwa haraka hivi. Hii ni fursa, Watanzania tujitokeze kupanda ndege hizi," amesema

Mwenzake, Augustine Rutasingwa amesema ni mara yake ya pili kutembelea nchi hiyo. "Mimi nilikuwa najaribu sikuwa najua kama nitashinda lakini nikaambiwa nimeshinda," amesema.

Chanzo: mwananchi.co.tz