Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ATCL kuanza safari za Dubai

ATCL ATCL CARGO TATU.jpeg ATCL kuanza safari za Dubai

Wed, 27 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) Mhandisi Ladislaus Matindi amesema kwa sasa kampuni hiyo inafanya kazi ya kuunganisha safari kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ukiwa kama kitovu cha mtandao wa safari zake na inatarijia kuanzisha safari za kwenda Dubai na London kuanzia Machi 31, 2024 baada ya safari za Johannesburg kurejeshwa.

Amesema hayo leo Machi 26, 2024 mkoani Dar es Salaam wakati wa mapokezi ya ndege mpya aina Boeing 737- 9MAX iliyotoka Seattle nchini Marekani.

Amesema ATCL inatarajia kuongeza vituo vya Lagos, Nigeria, Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Juba Sudan Kusini katika mtandao wake ili kuongeza ushindani.

Mhandisi Matindi ameongeza kuwa ATCL ili kukidhi mahitaji ya upanuzi wa mtandao wa safari zake, imewasilisha wizarani mapendekezo ya kuongeza ndege ya masafa ya kati katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2024/2025.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live