Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ASA yashauriwa kuongeza uzalishaji mbegu za alizeti

5f682eefc74de874411c074ed2831908.jpeg ASA yashauriwa kuongeza uzalishaji mbegu za alizeti

Wed, 17 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WAKALA wa Mbegu za Kilimo Tanzania (ASA), umeshauriwa kuongeza kasi zaidi kwenye uzalishaji wa mbegu ya alizeti kwa lengo la kumaliza tatizo la uhaba wa mafuta ya kupikia nchini.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Dk Christine Ishengoma alisema hayo juzi wakati kamati yake ilipotembelea wakala huo wenye makao yake mkoni Morogoro.

Kutokana na upungufu unaojitokeza, serikali imekuwa ikitumia fedha za kigeni kuagiza mafuta hayo kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kuziba pengo linalojitokeza.

Wajumbe wa kamati hiyo pia walikagua maabara ya mbegu za kilimo na ghala la kuhifadhia mbegu, na katika majadiliano waliushauri wakala huo pamoja na uzalishaji wa mbegu za mazao mengine, ujikite zaidi katika uzalishaji wa mbegu bora za alizeti.

Mjumbe wa kamati hiyo, JaneJelly Ntate, aliushauri wakala huo ujikite sasa kwenye kuzalisha kwa wingi mbegu ya alizeti kwani wakulima katika mikoa mbalimbali ukiwemo wa Dodoma wanahangaika kupata mbegu hizi baada ya kulima mashamba makubwa.

“ASA pamoja na kazi nzuri mnayoifanya mnazalisha mbegu nyingine , lakini mjikite sana kwneye mbegu za alizeti kuna shida sana ya utoshelevu wa mafuta ya kupikia na kwa kuwa wakulima wamejitokeza kwa wingi kulima zao hilo, wanakosa mbegu bora za alizeti,” alisema Ntate.

Mtendaji Mkuu wa ASA, Dk Sophia Kashenge alisema katika uzalishaji a mbegu za alizeti, waliongeza uzalishaji wa mbegu kutoka tani 111 mwaka 2018 na kufikia tani 243 mwaka 2019.

Dk Kashenge alisema kati ya kampuni 27 zinazozalisha mbegu ya alizeti, ni kampuni 19 zinazalisha mbegu ya Record ambayo ni mbegu iliyosafishwa na inayotoa kiwango kikubwa cha mafuta ya kupikia.

“Katika mazingira ya mkulima na matunzo ya kawaida ya shamba, mkulima anapata lita 25 hadi 36 na kilo 55 za seed cake kwenye kilo 100 za alizeti,” alisema Dk Kashenge mbele ya kamati hiyo.

Pamoja na hayo, aliwasilisha changamoto mbalimbali zinazoikabili wakala huo ikiwemo ya uvamizi wa mashamba na migogoro mingi ya ardhi hasa kwenye shamba la Msimba lililopo wilayani Kilosa mkoani Morogoro pamoja na uhaba wa maghala ya kuhifadhia mbegu zinazozalishwa.

Chanzo: www.habarileo.co.tz