Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ARU wasaini mkataba ujenzi wa majengo haya

ARU DEAN ARDHI ARU wasaini mkataba ujenzi wa majengo haya

Fri, 28 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

CHUO kikuu Ardhi kimesaini mkataba na kampuni ya China Jiangxi International Economic and Technical Coopertion kwaajili ya ujenzi wa majengo Mapya Manne yenye thamani ya Sh. Bilioni 32.9

Akizungumza katika hafla hiyo leo Julai 27, 2023 Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Evaristo Liwa Amesema mkataba huo ni utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya juu kwa mageuzi ya kichumi (HEET) ambao kwa ujumla Chuo kimepewa Tsh Bil 67.7

Ujenzi wa majengo hayo Manne kwa Kampasi kuu ya DSM ni utakamilika ndani ya miezi 18 na utaanza mwezi Agosti 2023.

Ujenzi huo utakapokamilika utakuwa na madarasa yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 4,604, Maabara mtambuka yenye uwezo wakuchukua wanafunzi 670, studios zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 780 na karakana za ufundi majengo zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 492.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live