Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ANSAF yataka mabadiliko tabia ya nchi yageuzwe fursa ya uzalishaji

85228 ANSADF+PIC.png ANSAF yataka mabadiliko tabia ya nchi yageuzwe fursa ya uzalishaji

Fri, 22 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkurugenzi mtendaji wa Jukwaa huru la kilimo (ANSAF), Audax Rukonge amewataka wadau wa kilimo na Serikali kuyatumia mabadiliko ya tabia nchi kama fursa ili kuongeza uzalishaji wa kilimo na kulinda mazingira. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Novemba 20,2019 jijini Dar es Salaam, Rukonge amesema mabadiliko ya tabia nchi ndiyo yatakuwa kiini cha mjadala katika mkutano ulioandaliwa na jukwaa hilo utakaofanyika jijini Dodoma Novemba 27 na 28, 2019.

“Tunajua Serikali ya awamu ya tano inahamasisha uchumi wa viwanda na malighafi za viwanda zinazotokana na kilimo. Kauli mbiu yetu ni kuangalia fursa na changamoto zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi.”

“Mabadiliko ya tabia nchi yanakuja na fursa mbalimbali ikiwa pamoja na kuwekeza kwenye uzalishaji wa mbegu zinazoweza kuhimili ukame, mbegu zinazoweza kuzalisha kwa muda mfupi, hiyo fursa,” amesema.

“Pia wataalamu waje na teknolojia ya utunzaji wa mazao, kuna miaka na misimu ambayo tutazalisha mazao mengi, lakini kama hatutakuwa na teknolojia ya utunzaji wa hayo mazao, mwaka unaofuata unaweza kuwa na mambo mabaya zaidi,” amesema

Ametaja pia fursa ya uvunaji wa maji ya mvua akisema ikitumika itasaidia kuhifadhi maji ya kutumia wakati wa ukame, baada ya kuyaachia yatiririke kwenda baharini. 

">Mbali na kuwekeza kwenye teknolojia, alisema kuna haja ya kuzihamasisha sekta binafsi ya jinsi ya kuchakata mazao ya kilimo.

Kuhusu upatikanaji wa mikopo na mitaji, amesema hiyo pia ni fursa inayopaswa kuangaliwa ili kusaidia miradi ya kilimo na usindikaji wa mazao.

Akizungumzia mkutano huo, Rukonge amesema katika mkutano huo, watajadili utafiti wa wataalamu kuhusu mabadiliko hayo ili Serikali na wadau wachukue hatua mahsusi.

“Mafanikio yaliyopo ni kwamba kwa saa polepole mabadiliko ya tabia nchi yameanza kusikika kwa watendaji wa Serikali. Tunataka wabunge, watunga sera na mawaziri walichukulie kwa uzito mkubwa katika utungaji wa sera, sheria na mikakati,” amesema. 

Amesema katika mkutano huo pia watazungumzia changamoto na sera za mabadiliko ya tabia nchi na kuangia fursa na changamoto zake.

“Lengo ni kuzungumza na wadau kuwa changamoto za mabadiliko ya tabia nchi ni halisi. Swali tunalouliza wadau ni kwamba tumejipanga namna gani? Je, tunaweza kuhakikisha kuwa viwanda ambavyo Serikali imekuwa ikihamasisha kujengwa havikosi malighafi vikashindwa kufanya kazi?” amehoji.

Chanzo: mwananchi.co.tz