Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ADC yasanua chanzo mradi wa BBT kufeli...

Ranch UFUGAJI MIFUGO ADC yasanua chanzo mradi wa BBT kufeli...

Fri, 22 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MWENYEKITI wa Chama ch ADC, Hamad Rashid Mohamed amesema mojawapo ya mapungufu yaliyojitokeza kwenye Mpango wa Jenga Kesho yako Iliyo bora (BBT), ni kitendo cha serikali kupitia wizara ya kilimo kutokuwa na mfumo sahihi wa kuwaingiza vijana kwenye mpango huo.

Amesema mpango huo licha ya kuwa na malengo mazuri, bado mambo mengi yamefichwafichwa huku wizara ikichukua vijana waliomaliza vyuo na wasiokuwa na kazi mitaani badala ya kuwaandaa vijana tangu wanapochagua fani za kusoma.

Hamadi Rashid ametoa kauli hiyo leo Ijumaa jijini Dar es Salaam wakati akichangia mada katika Kongamano la 4R za Rais Samia Suluhu Hassan lililoandaliwa na Shirika la Utangazaji Tanzania TBC. Ametoa mfano kuwa nchi za Mauritius na Maldives zimefanikiwa kushirikisha vijana na kupiga hatua kwenye sekta za uvuvu baada ya kuwasomesha na kuwawezesha vijana wenye mapenzi na shughuli za uvuvi.

BBT ni mpango ulioanzishwa na Wizara ya Kilimo kwa lengo la kukusanya vijana na kuwaweka kwenye makambi kisha kuwafundisha shughuli za kilimo, ufugaji na uvuvi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live