Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ACB kuwafikia watu 100,000 miezi 3 ijayo

Doro ACB kuwafikia watu 100,000 miezi 3 ijayo

Thu, 2 Sep 2021 Chanzo: ippmedia.com

Dora Saria, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa ndani ya wiki tatu za kwanza tangu huduma hiyo ianzishwe sokoni, imevutia maelfu ya watumiaji.

“Tunatarajia kuwafikia wateja zaidi ya 100,000 wa Akiba Wakala kwa wateja na wasio wateja. Kuchukuliwa kwa huduma hiyo imekuwa ya kushangaza machoni mwa watumiaji tangu kuanzishwa kwake karibu wiki tatu zilizopita;

Tumekuwa tukipokea maombi kadhaa ya kuanzisha maduka ya Akiba Wakala kutoka maeneo tofauti nchini ambapo huduma bado hazijatolewa. Hii inaonyesha kuwa huduma imekuwa ya kuvutia kwa umma kwa ujumla,” alisema Saria.

Katika kuongeza ufanisi wa benki hiyo, alisema ipo mbioni kufungua ukurasa mpya wa kibiashara kwa kujenga mfumo thabidi wa utoaji huduma kidijitali baada ya kupata mwekezaji wa kimkakati ambaye ni Benki ya Taifa ya Malawi (NBM).

Ubia huo kati ya ACB na NBM uliofikiwa hivi karibuni, unalenga kuijenga zaidi benki hiyo kwa kutanua mtandao wake wa kuduma za kifedha hapa nchini na kuhimili ushindani miongoni mwa watoa huduma. Ubia huo ni wa muda mrefu na tayari umeshaanza kuonesha matunda kama vile kuanzishwa kwa huduma ya Akiba Wakala.

“Benki imepata mwekezaji wa kimkakati, ambaye ni NBM. Tuna imani kwamba ubia huu utasaidia kupanua wigo wetu wa kibiashara ikizingatiwa NBM ni moja ya benki kubwa kwenye ukanda wetu wa nchi za kusini mwa Afrika;

"Ushirikiano tuliouanzisha kati yetu na NMB umeleta ari kubwa ambayo siyo tu ya kuhakikisha huduma za benki zinapatikana nchi nzima bali zinapatikana kidijitali na kwa uhakika,” alisema Saria.

Alisema mchakato wa kuibadili benki kuwa ya kidigitali unaendelea vizuri na tunauhakika utaleta unafuu na kuokoa gharama za upatikanaji wa huduma.

Kwa sasa benki inatoa huduma ya Akiba Mobile, ambayo inawezesha wateja wake kufanya malipo ya LUKU, ving’amuzi, muda wa maongezi pamoja na malipo yote ya serikali.

Akiba Mobile pia inapatikana kupitia mfumo wa USSD. Inamwezesha mteja kufanya miamala yake ya kibenki kupitia mawakala pia. Benki inatoa huduma nyingine za amana, mikopo, kuuza na kununua float, kutuma na kupokea fedha kupitia Western Union.

Alisema Benki ya Akiba siku zote imekuwa mstari wa mbele katika kufanya utafiti mbalimbali wa kuangalia mahitaji ya soko na wateja wake kwa ujumla, kwani inatambua umuhimu wa kutoa huduma zinazoendana na mahitaji ya soko.

Akizungumzia huduma ya Akiba Wakala ambayo imeanza kutolewa takribani wiki tatu sasa, Saria alisema tayari imeanza kutoa matokeo mazuri kwa kuwezesha wateja kupata huduma kwa urahisi zaidi popote pale walipo.

“Tunaamini kwamba kupitia huduma hii benki inakuwa mshiriki mzuri katika kuunga mkono harakati za serikali za kuhakikisha uwapo wa huduma jumuishi za kifedha yaani kwa Watanzania wote.

"Tumeingia sokoni na jumla ya wakala wapatao 200 na lengo letu ni kuendelea kuongeza wakala wengi kadri iwezekanavyo kwa lengo la kukidhi kiu ya upatikana wa huduma hii nchi nzima bila ulazima wa mteja kuja kwenye matawi ya benki,” alifafanua.

Chanzo: ippmedia.com