Menu ›
Biashara
Tue, 21 Nov 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Ukuaji wa teknolojia katika masafa ya intaneti umeongezeka ambapo kwa sasa minara ya kutoa huduma ya 5G imefikia 300 na hivyo kuwawezesha watanzania kupata huduma kwa kasi ya hali ya juu.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) Justina Mashiba ametoa tathmini hiyo wakati akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kuhusiana na utendaji wa mfuko huo.
Mashiba amesema, Mfumo wa upatikanaji wa intaneti ya 5G unawawezesha watanzania hasa wanaoishi kwenye miji mikubwa kuwa na mtandao wa kisasa wa intaneti na kuwawezesha kuwasiliana kwa uharaka na ufanisi mkubwa.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live