Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

20 wahitimu kurusha drones kuboresha shughuli za kilimo

20 Wahitimu Kurusha Drones Kuboresha Shughuli Za Kilimo 20 wahitimu kurusha drones kuboresha shughuli za kilimo

Thu, 25 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanafunzi 20 wamehitimu Kozi ya Mafunzo ya Kurusha Ndege Zisizo na Rubani katika Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) ikiwa ni sehemu ya Mradi wa Kuimarisha Huduma za Afya ya Mimea nchini Tanzania kwa ajili ya kuhakikisha Usalama wa Chakula.

Mahafali hayo yamefanyika katika viwanja vya Makao Makuu ya TCAA Banana - Ukonga ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa ushirikiano wa kimaendeleo wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Cedric Merel ambao ndio wadhamini wakuu wa mradi huu utakaotekelezwa kwa miaka mitatu unaolenga kutatua mapungufu ya kiuendeshaji na ya kiufundi yanayohusiana na afya ya mimea ambayo yanazorotesha biashara ya kilimo na kuhatarisha usalama wa chakula nchini Tanzania.

Wengine waliohudhuria Mahafali hayo ni na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Chakula Duniani (FAO) Dkt. Nyabengi Tipo, Mkurugenzi Idara ya Kilimo na Usalama wa Chakula -SMZ Hamad Masoud, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Daniel Malanaga, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Udhibiti wa Viuatilifu Tanzania (TPHPA) Prof. Joseph Ndunguru na Mkuu wa Chuo cha Usafiri wa Anga (CATAC).

Mradhi huu umeratibiwa na Umoja wa Ulaya(EU) kwa kushirikiana na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) pamoja na Wizara ya Kilimo Nchini kupitia Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania (TPHPA).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live