Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Whyte amwaga wino kuzichapa na Fury

Dillian Whyte Tyson Fury.jpeg Dillian Whyte asaini mkataba kuzichapa na Tyson Fury

Tue, 22 Feb 2022 Chanzo: eatv.tv

Hatimaye Bondia Dillian Whyte ametia saini kandarasi ya pambano atakalopigana dhidi ya Tyson Fury kuwania taji la uzito wa juu Duniani la WBC kwenye Uwanja wa Wembley nchini England baadae mwaka huu.

Pambano hilo limepangwa kufanyika Tarehe 23 mwezi Aprili mwaka huu licha ya Whyte kuchelewa kuweka saini hadi dakika za mwishoni baada ya Gypsy King kumkejeli ikiwa ni saa chache kabla ya tarehe ya mwisho ya kufikia makubaliano. Kulikuwa na hofu kwamba Whyte huenda asikubaliane na mpango wa pambano hilo kutokana na mzozo wa mgawanyiko wa maslahi ambao unaoneakana kumpendelea mpinzani wake kwa viwango vya 80 kwa 20.

(Tyson Fury bingwa wa uzito wa juu duniani wa WBC)

Sasa imethibitika kwamba mabondia hao wote wawili wamemwaga wino kwenye kandarasi za pambano hilo ambalo litafanyika kwenye uwanja wa Wembley jijini London nchini England. Siku ya mwisho ya kutia saini kandarasi hiyo ilipowadia hapo jana, Fury alienda kwenye mitandao ya kijamii na kumwambia Whyte achague kutia saini mkataba huo au kama hataki basi aondoke kabisa.

Promota wa Gypsy King Frank Warren alishinda haki ya kuendeleza pambano hilo kwa kitita cha paundi milioni 30, ambalo lilithibitishwa kuwa ndio dau kubwa zaidi katika historia ya mapambano ya uazani huo. Lakini Whyte ameamua kukaa kimya, huku promota mwenza wa Fury kutoka Marekani, Bob Arum akidai kuwa Brixton 'Body Snatcher' amekuwa akiomba pesa zaidi ili kulitangaza pambano hilo.

Chanzo: eatv.tv