Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wanyonyi: Mleteni huyo Mandonga

Mandonga Amchapa Mganda Na Kutwaa Taji Lake La Kwanza Kwenye Ndondi Wanyonyi: Mleteni huyo Mandonga

Thu, 30 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kumkung’uta propa Charles Kakande wa Uganda, bondia Daniel Wanyonyi sasa anamtaka tena bondia mwenye tambo kibao, Karim Mandonga Mtu Kazi wa Bongo.

Wanyonyi alitumia dakika mbili tu kumcharaza Kakande aliyeshindwa kustahimili makonde mazito na kumlazimisha refa kusimamisha pigano hilo la uzito wa light heavy.

“Nimerudi fomu yangu ya zamani na nitapita na yeyote akiwemo Mandonga,” alisema Wanyonyi aliyeonekana kaiva kinyama.

Ni ushindi ambao ulionekana kumpatia Wanyonyi bonga points, aliyejipiga kifua kwa hasira ishara kwamba yuko tayari kumalizana na mpinzani yeyote atakayesimama mbele yake.

Lakini Mandonga aliyetumia staili yake mpya ya Mbungambunga kumkomoa Kenneth Lukyamuzi, aliudhihaki ushindi wa Wanyonyi akidai alikutanishwa na bondia ‘mzee’.

“Wanyonyi amepewa mzee, mleteni niko tayari kukutana naye kwa mara nyingine na atake asitake nitampiga tu,” Mandonga alijigamba.

Katika pigano lake dhidi ya Lukyamuzi, Mandonga alijikaza sana akitumia kila aina ya mbinu kumzima mapema mpinzani wake lakini bila kufaulu.

Lukyamuzi alitumia ngumi fupi za tumbo na kichwa na kumfanya Mandonga kuinamisha kichwa kila mara hivyo kumpatia refa wa pigano hilo wakati mgumu wa kuwatenganisha kila mara.

Lakini kimo kirefu cha Mandonga ulichangia ushindi wake kwani alimwahi mpinzani wake ngumi za kicha na uppercuts zilizomfanya Lukyamuzi kurudi nyuma.

Katika pigano hilo, jaji Abdallah Mgai wa Uganda alitoa uamuzi wa 74-78 huku Anthony Rutta wa Bongo akitoa maamuzi wa 77-75 naye Linda Abok akitoa uamuzi wa 77-75 na kumtawaza Mandonga mshindi kwa alama chache.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live