Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wadau ngumi wapinga tamko la BMT

43833 Pic+ngumi Wadau ngumi wapinga tamko la BMT

Tue, 26 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Muda mfupi baada ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kutangaza Machi 30 kufanyika uchaguzi wa Bodi ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC), wadau wa mchezo huo wamepingana na baraza hilo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa BMT, Najaha Bakari alitangaza Machi 25 kuwa mwisho wa kuchukua fomu za uongozi huku wagombea wakifanyiwa usaili Machi 29.

“Kampeni zitafanyika baada ya usaili (Machi 29) tayari kwa uchaguzi (Machi 30), alisema Najaha.

Hata hivyo, muda huo wa kampeni umepingwa na baadhi ya wadau wa ngumi na wengine wameeleza wasiwasi wa huenda viongozi wa bodi hiyo wameandaliwa.

“Hata uchaguzi wa nchi unatoa nafasi ya kampeni, sijui kwenye ngumi wamewaza kitu gani, wajaribu kuliangalia hili kwa faida ya ngumi,” alisema promota wa mchezo huo, Juma Ndambile.

Ndambile alisema kitendo cha BMT kutotoa muda wa kutosha wa kampeni, ana wasiwasi kuna watu wameandaliwa kuwa viongozi wa bodi.

Bondia nguli Mada Maugo alisema muda wa kufanyiwa usaili wagombea na siku hiyo hiyo wafanye kampeni ni kitu ambacho hakiwezekani.

“Hatuna haraka, kama BMT inataka basi itoe japo siku 15 au 10 kwa ajili ya wagombea kujinadi, tuwasikilize na tuwafahamu kabla ya kupiga kura,”alisema Maugo.

Katibu Mkuu wa PST, Anthony Rutha alisema uchaguzi huo una nia njema, lakini wasimamizi walipaswa kutoa muda kwa wagombea kujinadi.

Bondia Japhet Kaseba alisema kuwa BMT ilipaswa kutoa muda wa siku chache ili wapiga kura wawafahamu wagombea wao, wana sera gani na si kuwafahamu ukumbini siku ya kupiga kura.

Nafasi zinazogombewa ni rais, makamu wa rais, katibu mkuu na mweka hazina. Baadhi ya sifa za mgombea ni kuhitimu elimu ya shule ya msingi, kujua kusoma na kuandika.



Chanzo: mwananchi.co.tz