Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vita ya Ukraine, yawapa presha mabondia Bongo

Blog TypeOfGloves 1 Vita ya Ukraine, yawapa presha mabondia Bongo

Sat, 5 Mar 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Vita ya Russia dhidi ya majirani zao wa Ukraine vimewatia hofu mabondia nchini wakielezwa kuhofia soko lao la ngumi za kulipwa kuporomoka kutokana na vita hivyo vinavyoiponza Russia kuwekewa vikwazo kila kona, ikiwamo wasimamizi wa michezo duniani.

Soko kubwa la ndondi kwa mabondia Watanzania liko nchini Russia kwa muda mrefu huku wale wanaofanya vizuri akiwamo, Twaha Kiduku, Abdallah ‘Dullah Mbabe’ Pazi, Mfaume Mfaume na wengine wengi wakiwa na rekodi ya kucheza mapambano kadhaa nchini humo kwa nyakati tofauti.

“Kiduku na Mbabe ndiyo mabondia Watanzania ambao wamewahi kulipwa pesa nyingi kwenye mapambano ya Russia, ingawa asilimia kubwa ya mabondia nchini soko lao liko Russia, Marekani na Uingereza,” alisema kaimu rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa (TPBRC), Agapeter ‘Mnazareth’ Basil.

Kiduku, bondia namba moja kwenye uzani wa super middle alisema pamoja na baadhi ya rafiki zake nchini Russia kumpa matumaini ya kuwa wako salama na shughuli zinaendelea lakini bado yuko mguu ndani mguu nje kwenda kucheza kwa sasa nchini humo kama ikitokea akapata pambano huko.

“Hiki kinachoendelea kati ya nchi hiyo na Ukraine ni cha kuwaombea tu kipite, maisha mengine yaendelee, kwani kuna baadhi yetu pia kitatuathiri kwa namna moja au nyingine, ukizingatia moja ya nchi ambazo Watanzania tunakwenda kupigana sana ni Russia,” alisema Kiduku na kuongeza.

“Kwenye mapambano yao kule wanalipa masilahi mazuri, ingawa inategemea na utakavyozungumza nao, binafsi nilipocheza nililipwa pesa nzuri, japo nao pia hawamchukui bondia tu ili mradi uwa wanaangalia rekodi yake,”.

Bondia wa zamani, Chaurembo Palasa alisema vita hiyo ni tatizo kubwa.

Chanzo: Mwanaspoti